Jumatatu 10 Novemba 2025 - 21:16
Utawala wa Kizayuni ndio Unao Tekeleza Ugaidi na Mateso katika Ukingo wa Magharibi

Hawza/ Harakati ya Hamas imetangaza kuwa takwimu za Umoja wa Mataifa kuhusu uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi ni ushahidi wa wazi wa siasa ya mauaji na mateso inayotekelezwa na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Harakati ya Muqawama ya Hamas siku ya Jumamosi ilitoa tamko ikisema kuwa usajili wa zaidi ya mashambulizi 260 yaliyofanywa na walowezi wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina, na mali zao katika Ukingo wa Magharibi uliokaliwa kwa mabavu ndani ya mwezi wa Oktoba pekee na Umoja wa Mataifa — na karibu mashambulizi 1500 tangu mwanzo wa mwaka — ni ushahidi wa wazi wa siasa ya mauaji na mateso ya kimfumo inayofuatwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina; siasa ambayo inalenga kuwafukuza watu kutoka katika ardhi yao na kulazimisha uhalisia wa kikoloni na kibaguzi unaojengwa juu ya utawala na vitisho.

Katika tamko hilo la Hamas imesemwa kuwa: kulenga mashamba ya kilimo wakati wa msimu wa mavuno ya zeituni, kwa namna ya makusudi na ya kurudiarudia, ni jaribio la kuwashinikiza wakulima wa Kipalestina; tendo linalotekelezwa ndani ya mpango wa wavamizi wa kutekeleza sera ya kuwahamisha Wapalestina, kupanua makazi ya walowezi na kuimarisha udhibiti wao juu ya Ukingo wa Magharibi.

Harakati ya Hamas imezitaka jumuiya za kimataifa, Umoja wa Mataifa na pande zote husika kutekeleza wajibu wao wa kisheria na kimaadili, kulaani uvamizi huo, na kuchukua hatua za kuzuia ugaidi wa walowezi pamoja na uvamizi uliopangwa dhidi ya taifa la Palestina katika Ukingo wa Magharibi. Pia imesisitiza haja ya kuwafikisha viongozi wa utawala wa Kizayuni katika mahakama za kimataifa kutokana na uhalifu wao unaoendelea dhidi ya taifa, ardhi na maeneo matakatifu ya Palestina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha